Cheki
taswira, kinda wa Azam FC, Farid Mussa akiwa katika majaribio kuwania
nafasi acheze soka la kulipwa barani Ulaya. Hapa Farid anafanya
majaribio katika klabu ya Club Deportivo Tenerife Hispania. Leo
ametimiza siku ya nne katika majaribio na taarifa zinasema anaendelea
vizuri.
Awali,
Farid alisema ana imani kubwa kwamba atapasi majaribio hayo kwa kuwa
ndiyo kitu alichokuwa anakihitaji na atakipigania kwa nguvu zote.
Hata
hivyo, Farid alikubali kwamba anaona Hispania wamepiga hatua kubwa
kimaendeleo katika soka, jambo ambalo ni zuri kwake kwa kuwa atajifunza
zaidi.
PICHA KWA HISANI YA AZAM FC.
Post a Comment