0



Azam TV wataionyesha moja kwa moja mechi kati ya Azam FC dhidi ya Simba. Mechi inayosubiriwa kwa hamu kuu.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ni muhimu zaidi na maradufu kwa Simba. Kwa kuwa kama itapoteza mechi hiyo, itakuwa imejiondoa rasmi katika mbio za ubingwa.

Simba ina pointi 57 katika nafasi ya tatu, Azam FC ina 58 katika nafasi ya pili. Simba inahitaji kushinda ili kuendelea kuwa katika mbio hizo.


Kama itaishinda Azam FC itakuwa imefikisha pointi 60 na kupanda hadi nafasi ya pili. Kwa kuwa Yanga ndiyo vinara na tayari wana pointi 62 kabla ya kuivaa Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kesho. 

Post a Comment

 
Top