Polisi nchini
Uganda wamemfungulia mashtaka kiongozi wa upinzani daktari Kiiza Besigye
kwa kujaribu kuingia jijini Kampala kwa msafara wa magari
Msemaji
wa polisi anasema kuwa kiongozi huyo wa upinzani alikaidi amri ya
kutoingia mjini Kampala kufuatia maelfu ya mashabiki wake kuzingira gari
lake huku wengine wengi wakimfuata na kuunda msafara wa magari.
Uganda yamfungulia Besigye mashtaka
Polisi wanasema kuwa Besigye alikuwa amepewa idhini
ya kuhudhuria hafla ya maombi katika makao makuu ya chama chake ilimradi
tu asivuruge amani na utangamano mjini Kampala.
Hata hivyo polisi walimzuia alipokuwa katika makutano ya barabara za Mulago na Wandegeya karibu sana kuingia mjini.
polisi walimzuia alipokuwa katika makutano ya barabara za Mulago na Wandegeya
Mwandishi wa BBC aliyeko Kampala Patience Atuhaire anasema polisi wamezuia watu kufuata gari la kiongozi huyo wa chama cha FDC.
Polisi wametumwa kwa wingi eneo hilo.
Gari la Bw Besigye lilibururwa na gari la polisi na kuelekezwa kituo cha polisi cha barabara ya Kira.
Gari la Bw Besigye lilibururwa na gari la polisi na kuelekezwa kituo cha polisi cha barabara ya Kira.
Bw Besigye ambaye amekuwa katika kifungo cha
nyumbani alikuwa ndio anatoka nyumbani kwake kwa mara ya kwanza hii leo
tangu uchaguzi kufanyika nchini Uganda.
Kiongozi huyo wa upinzani
alimaliza katika nafasi ya pili lakini akapinga matokeo hayo ya uchaguzi
akisema kuwa rais Museveni alikuwa amefaidika na udanganyifu mwingi na
kuwa uchaguzi huo haukuwa wa uhuru wala haki.
Post a Comment