Wakati Atletico Madrid akijiandaa kwa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona, kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ameonesha uwezo wake wa kusakata kambumbu wakati kikosi chake kikifanya mazoezi kwenye uwanja wa Nou Camp.
Simeone, 45, ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo, amedhihirisha bado yuko vizuri pale alipoamua kuonesha mautundu ya kuuchezea mpira.
Atletico Madrid wanaingia kuikabili Barcelona wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mkubwa kwenye mchezo wao uliopita wa ligi wa magoli 5-1 dhidi ya Real Betis wakati Barcelona wao wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kuchezea kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Real Madrid ikiwa ni kipigo cha kwanza baada ya kucheza mechi 39 (kwenye mashindano yote) bila kupoteza.
Habari mbaya kwa upande wa Atletico Madrid ni kukosekana kwa wachezaji wao wawili Stefan Savic na Jose Gimenez ambao ni majeruhi lakini nafuu yao ni urejeo wa Diego Godin.
Barcelona itakuwa mwenyeji wa Atletico Madrid kwenye mchezo wa leo wa Champions League hatua ya robo fainali ikiwa ni mchezo wa kwanz kabla ya timu hizo kurudiana baada ya majuma mawili kwenye uwanja wa Vicente Calderón. Mechi ya leo inatarajiwa kuanza saa 3:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Post a Comment