Hatua ya mchezaji
maarufu wa soka duniani Lionel Messi kutoa viatu vyake viuzwe kusaidia
watu wasiojiweza imeibua mjadala mkali nchini Misri.
Wakati wa mahojiano ya runingani ''katika kipindi cha Yes am Famous'' kinachopeperushwa hewani na runinga ya MBC Misri, mchezaji huyo wa Argentina aliwaambia watangazaji hao kwamba angependa kutoa viatu vyake vipigwe mnada.
Kitendo chake kilipokelewa tofauti kabisa na wiki chache zilizopita alipopongezwa na kusifiwa sana kwa kutimiza ndoto ya kijana mmoja wa Afghanistan alipomtumia mpira na fulana yake.
Muda mfupi baadaye wakazi wa maeneo hayo walimkashutumu sana kupitia mitandao ya kijamii.
Post a Comment