0

Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria wasanii ambao watakiuka agizo la kufanya video za muziki na kuzitoa bila kukaguliwa na Bodi ya Filamu ili zikaguliwe.
Ali Kiba, AY, Diamond na Navy Kenzo
Akiongea na Bongo5, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya wasanii kuendelea kufanya kazi zao za muziki bila kufuata taratibu.

“Taratibu zinaeleza wazi, kwamba kabla ya kushoot video yako unatakiwa upeleke script ikaguliwe kwanza na baada ya hapo utapewa ruhusa ya kuendelea,” alisema Msalla.

“Sasa hivi tutakuwa wakali kweli hili, hili ni swala la kisheria taratibu ziko hivyo, kwa hiyo nikufuata taratibu tu,” aliongeza.

Kwa upande wa Mwanasheria wa Wizara ya Habari amesema msanii kuendesha kazi bila ya kuzingatia sheria ni kosa huku akiwataka wasanii kupeleka kazi zao Bodi ya Filamu kukaguliwa kabla ya kutoka.

“Snura hajajisajiri, ametoa kazi bila ya kupata kibali pamoja na kuitoa nyimbo bila ya kuipeleka sehemu husika kwa ajili ya kuifanyia ukaguzi ili kuithibitisha kama inafaa,” Mwanasheria alimtolea mfano Snura.

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!Share

Post a Comment

 
Top