WCB imemzawadia gari jipya msanii wake, Harmonize.
Bosi wake, Diamond, ameandika kwenye Instagram: Kama nikusiivyo siku
zote ni juhudi na nidhamu yako ndio itayokufanya upate matunda ya kazi
yako….. Usiache unyenyekevu, kuheshimu mkubwa na mdogo, kumuomba na
kumshukuru Mwenyez Mungu kwa kila hatua ndogo Uipigayo…. Congrats kwa
your New Ride.”
Naye Harmonize hakuacha kuonesha furaha yake.
“Nichukue fursa fupi kuushukuru uongozi wangu mzima wa @wcb_wasafi
@mkubwafella @babutale @sallam_sk @ricardomomo @diamondplatnumz kwa
kunijali na kunithamini kijana wao wakanizawadia gari daaaaah furaha
niliyo nayo haielezeki,” ameandika msanii huyo.
“Kwakweli nina furaha na ninashukuru sanaa nina mengi ya kuongea
lakini sizani kama nikianza kuandika nitamaliza kubwa ni kwamba
namshukuru m/mungu nashukuru kwa kurudia tena uongozi wangu @wcb_wasafi
kwa zawadi lakini nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipo washukuru wazazi
wangu walio nizaa na kunilea hadi nikafikia hapa na shukrani za dhati
ziwafikie mashabiki zangu ambao wapo bega kwa bega kunisupport katika
kazi zangu pia mama naseeb umekuwa ukinisistiza na kunisihi jinsi ya
kuishi na watu @kendrah_michael.”
“Nimalize kwakusema ninashukuru sanaa na nina amini kuna
mengi mazuri
zaidi yapo mbele ila asieshukuru na kidogo kamwe hatoshukuru na kikubwa
thanks #allah thanks #wcb #thanks #mashabiki.”
Jiunge na Bongo5.com sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata
habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote
kali kutoka Bongo5!Share
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment