MADRID, HISPANIA
BINGWA wa tenisi katika michuano ya wazi ya Barcelona, Rafael Nadal, raia wa nchini Hispania, amekabidhiwa bendera ya nchi hiyo kwa ajili ya kuwakirisha katika michuano ya Olympics nchini Brazil ikiwa na ujumbe wa kupinga madawa.Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zinatarajiwa kufunguliwa Agosti 5 mwaka huu katika Uwanja wa Maracana, ambapo kutakuwa na mashindano mbalimbali.
Hii ni mara ya pili kwa Nadal kushinda mashindano ya Grand Slam na kupewa bendera ya nchi kwa ajili ya kuwakilisha.
“Hii ni fulsa moja wapo ya kuwakirisha nchi, ninaamini nitarudi na ubingwa kwa ajili ya nchi yangu. Nina furaha kubwa kupewa bendera ya nchi kwa ajili ya kupinga matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu michezoni ikiwa siku chache nilituhumiwa kutumia madawa wakati sio kweli,” aliandika Nadal kwenye akaunti yake ya Instagram.
Post a Comment