NEW YORK, MAREKANI
BONDIA Floyd Mayweather, ameonesha jeuri ya fedha kwa kununua gari mbili aina ya Bugatti Veyron zenye thamani ya pauni milioni 4.Kupitia akaunti yake ya Instagram, bondia huyo aliweka picha yake huku akiwa anazionesha gari hizo.
“Haya ni maisha yangu ya kawaida na ya kila siku, sina cha kufanya zaidi ya kutumia fedha zangu, nilianza kuwekeza tangu nikiwa kwenye ngumi hivyo nitaendelea kutumia fedha,” aliandika Mayweather.
Bondia huyo anaongoza kwa kuwa na magari ya kifahari ambayo ni Bugatti Veyrons na Bugatti Veyron Grand Sport, Ferrari 458 Spiders na Lamborghini Aventador, Porsche 911 Turbo S na Ferrari 599 GTB Fiorano.
Lakini kati ya gari zake zote Bugatti Veyron ina kazi ya 267 mph, pia ni ghari zaidi kuliko zingine.
Post a Comment