0
Kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kikishirikiana na kikosi cha serikali ya Mogadishu vimefanikiwa kuyakomboa maeneo mengi yaliyokuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo wa al-Shabab. 

Ripoti kutoka Somalia zinasema kuwa, vikosi hivyo vimepata mafanikio katika operesheni zao za hivi karibuni dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab na kuyakomboa maeneo mengi yaliyokuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo hao.

kwa mujibu wa maafisa wa kijeshi wa AMISOM ni kuwa, wanamgambo wa al-Shabab wamelazimika kuondoka katika maeneo mengi yaliyokuwa ni ngome zao kutokana na kuandamwa na operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi yao.

Kikosi cha kusimamani amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kinachoundwa na nchi za Kenya, Ethiopia, Uganda na Burundi kimekuwa nchini Somalia tangu mwaka 2007.
Licha ya mafanikio hayo ya AMISOM na kikosi cha serikali ya Somalia, lakini wanamgambo wa al-Shabab wangali wanatekeleza mashambulio ya hapa na pale katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kusababisha mauaji ya watu.

Ikumbukwe kuwa, askari 15 wa Somalia waliuawa katika shambulio la jana la wanamgambo wa al-Shabab katika mji wa Runirgood kaskazini mashariki mwa mji mkuu Mogadishu.

Post a Comment

 
Top