0
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran asubuhi ya leo amempokea rasmi katika ikulu ya Sa'dabad Bi Park Geun-hye Rais wa Korea Kusini.

Baada ya hafla ya mapokezi iliyoambatana na kupigwa nyimbo mbili za taifa la Iran na Korea Kusini Marais hao walianza mazungumzo ya pande mbili.

Aidha baada ya kumaliza mazungumzo hayo, Marais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu na Park Geun-hye wa Korea Kusini wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja na waandishi wa habari.

Rais Park Geun-hye wa Korea Kusini aliwasili jana hapa mjini Tehran kwa ziara rasmi ikiwa ni katika kujibu mwaliko wa rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Park Geun-hye ni rais wa kwanza wa Korea Kusini kuitembelea Iran baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika safari yake hii Rais huyo anaongoza ujumbe wa watu zaidi ya 200 wanaojishughulisha na masuala ya kiuchumi kutoka mashirika tofauti ya serikali na sekta binafsi.

Post a Comment

 
Top