Klabu ya soka ya Leicester City
wameshinda taji la ligi kuu England katika historia inayovutia kwenye
ligi hiyo. Suluhu ya 2-2 waliyoipata Tottenham dhidi ya Chelsea siku ya
jumatatu usiku ilisababisha mafanikio hayo makubwa kuwahi kutokea kwa
upande wa Claudio Ranieri.
Lakini wamepoteza michezo mitatu tu katika kile kinachotafsiriwa kama hadithi za kale na ushindi wa kipekee katika timu hiyo. Wapinzani wao wa karibu Spurs,Arsenal,Manchester City, Manchester United na washindi wa ligi msimu uliopita Chelsea wameshindwa kuwazuia mbweha katika msimu mzima wa ligi.
Washindi wapya
1
Leicester City ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza mara ya kwanza kabisa-
5,000-1 uwezekano wao wa kushinda ligi msimu ulipoanza
-
2-2 matokeo ya mechi kati ya Chelsea na Tottenham ambayo iliwazawadi Leicester taji la ligi
-
Rais wa shirikisho la soka duniani Gianni Infantino amesema historia nzuri ya Leicester ilikua ni kama hadithi za kale.
Post a Comment