0



CHAMA cha Mpira wa Wavu Nchini (TAVA) kimeanza mikakati ya kuhakikisha inaingia timu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2020 itakayofanyika Japan.

Wavu hawatakuwa na timu katika michuano ya mwaka huu inayotarajiwa kufanyika kwa wiki mbili kuanzia Agosti 5 huko Rio de Janeiro, Brazil.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TAVA, Muharami Mchume, hatua ya kwanza ya mikakati ya kuhakikisha Tanzania inaingiza timu ya wavu Japan ni kuandaa mafunzo ya walimu wa wavu wa ufukweni.
Amesema tayari zaidi ya washiriki 20 wameshajiandikisha kwa mafunzo hayo yafanyika kwa wiki moja kuanzia Novemba 11 kwenye Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu, Dar es Salaam. Kozi hiyo itashirikisha walimu wa shule za msingi na sekondari na kwamba walimu kutoka Kinondoni, Temeke na Ilala wamejiandikisha kwa wingi.

Washiriki wanatarajiwa kunolewa na mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Wavu (FIVB), Papageorcious Alexis. Alisema huo utakuwa msingi wa kuiwezesha Tanzania kushiriki kwa mara ya kwanza wavu wa ufukweni katika Michezo ya Olimpiki.

Post a Comment

 
Top