Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kwa makamu mwenyekiti wake Jerome Msemwa,
April 3 imetoa tamko kuhusu zile tuhuma za upangaji wa matokeo kwa
mechi za Ligi daraja la kwanza zilizokuwa zinazihusisha timu za kundi C.
Timu za Geita Gold ya Geita, JKT Oljoro ya Arusha na Polisi Tabora ya Tabora zimekutwa na hatia ya kosa la upangaji matokeo na hivyo zote zimeshushwa Ligi daraja la pili na JKT Kanembwa imeshushwa hadi Ligi ya mkoa sababu tayari ilikuwa imeshuka kutoka Ligi daraja la kwanza..
Kamati ya nidhamu pia imewafungia refa Saleh Mang’ola na kamisaa wa mechi ya JKT
Kanembwa dhidi ya Geita Gold Moshi Juma kutojihusisha na soka maisha, na kamati pia itatangaza baada ya kupitia kanuni ni timu ipi imepanda Ligi kuu na ipi imepanda daraja la kwanza.
Hii ni List ya watu wote waliokumbana na adhabu ya kamati ya nidhamu

- Kocha msaidizi wa Geita Gold Choke Abeid amefungiwa maisha kutojihusisha na soka.
- Magolikipa Mohamed Mohamed wa JKT Kanembwa na Dennis Richard wa Geita Gold wamefungiwa miaka 10 na faini milioni 10 kutojihusisha na soka.
- Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora, Fateh Remtullah, Mwenyekiti wa klabu ya JKT Oljoro, Amos Mwita na kocha msaidizi wa Polisi Tabora, Bernad Fabian wamefungiwa maisha kutojihusisha na mpira wa miguu.
- Mwamuzi wa mchezo kati ya Polisi Tabora v JKT Oljoro, Masoud Mkelemi na mwamuzi wa akiba, Fedian Machunde wamefungiwa kwa muda wa miaka kumi kutojihusisha na mpira wa miguu, na kutozwa faini ya shilingi milioni (10,000,000) kumi kila mmoja.
Post a Comment