0

Mahakama ya katiba Korea kusini imeendelea kukataa rufaa iliyowasilishwa kupinga sheria inayopiga marufuku biashara ya ngono ikiwa ni ishara ya kushindwa kwa wafanyabiashara hii ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakifanya kampeni kupinga hayo maamuzi.

Hakimu Kim chang jong amesema kampeni za kuleta uwazi na uhuru katika ngono hazimaanishi kuwa biashara inayohusisha ngono ni kitu halali, sheria ambayo ilipitishwa mwaka 2004 inasema watu wanaofanya biashara ya kujiuza na wateja wao watahukumiwa kulipa faini au kutumikia 

kifungo cha hadi mwaka mmoja gerezani endapo watakutwa na hatia ya kujihusisha na biashara hii.
kora 

Haya maamuzi yaliungwa mkono na majaji wengine watano kwenye mahakama ya katiba ya korea ya kusini ambapo hata hivyo upinzani mkubwa kwa sheria hii ulionekana toka kwa majaji wengine watatu ambapo mmoja alipinga kuharamishwa kwa  biashara ya ngono akisema kuwa sheria hiyo inaathiri mustakabali wa baadhi ya wanawake ambao hutegemea biashara hii kuendesha maisha yao.

Majaji waliounga mkono kuhalalishwa kwa biashara hii wamesema kuwa si kweli kwamba biashara ya ngono inashusha utu au hadhi ya ubinadamu kwani tishio la ustawi wa uhai wa mtu pale 

anapokosa shughuli ya kuendesha maisha yake ndio kitu kinachoshusha utu wa mwanamke zaidi ya biashara ya ngono.

Mwaka jana Mahakama hii ya katiba ilifanya maamuzi ya kihistoria wakati ilipopitisha sheria ya kuhukumu kosa la zinaa kwa kifungo cha miaka miwili yakiwa maamuzi yaliyoakisi mtazamo hasi wa jamii ya korea ya kusini katika masuala ya kijamii ikiwemo ngono.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top