Maafisa wakuu wa idara ya usalama nchini Nigeria wanasema kuwa wamkamata kiongozi wa kundi la kiislamu la Ansaru.

Kundi hilo linauhusiana na mtandao wa ugaidi wa Al Qaeda.

Msemaji wa idara ya ulinzi Brigedia jenerali Rabe Abubakar amesema kuwa Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la kati la Kogi.

Khalid alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa mtandao huo wa ugaidi ambao walikuwa katika orodha ya wahalifu wanaotafutwa na Marekani.

Dola milioni 5 pesa za Marekani zilikuwa zimeahidiwa mtu yeyote atakayetoa habari kuhusi wapi aliko.
Ansaru ni kundi lililojitenga na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Ansaru ni kundi lililojitenga na wapiganaji wa kundi la kiislamu la Boko Haram.
Linatuhumiwa kwa kuwateka nyara raia wa kigeni mbali na mauaji ya wageni kadhaa.
Kundi hilo linakumbukwa kwa shambulizi la kuvizia dhidi ya gereza moja mjini Abuja katika mwaka wa 2012 ambapo wafungwa waliohusiana na kundi hilo waliachiwa huru.