Azam FC imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji wake Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo.
Sare hiyo inaifanya Azam FC kuangusha pointi mbili kutokana na sare hiyo mjini Mwanza. Hiyo ni nafuu kubwa kwa Simba.
Azam
FC ilikuwa inafukuzia pointi 9 katika mechi zake tatu za kiporo, lakini
sare hiyo inaifanya iwe imedondosha pointi mbili baada ya sare hiyo
kwenye uwanja uliojaa maji na tope.
Sare
inaifanya Azam FC kuwa na pointi 51, inaendelea kubaki katika nafasi ya
tatu na Yanga inakuwa katika nafasi ya pili baada ya kushinda leo bao
3-1 dhidi ya Kagera Sugar, sasa ina pointi 53.
Simba
iko kileleni ikiwa na pointi 57 lakini imecheza mechi mbili zaidi ya
Yanga na Azam FC ambazo kila moja ina mechi 22 na Simba imecheza 24.
Kama Azam FC itashinda mechi zake mbili zijazo, ndiyo itakuwa na pointi 57, sawa na Simaba na kama itapata sare nyingine, maana yake haitaweza kuifikia Simba
Post a Comment