Jeshi la Syria
limegundua kaburi lenye mabaki ya miili kama 40 katika mji wa Palmyra,
ambao ulikombolewa kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State, awali juma
hili.
Palmyra ilikuwa mikononi mwa IS kwa karibu mwaka mzima, na wakati huo, wapiganaji hao waliuwa watu wengi.
Kati yao ni wanaume 25 waliouwawa katika uwanja maalumu uliojengwa zama za Wa-rumi katika mji huo wa kale.

Post a Comment