Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Equitorial Guinea
yanaonyesha kuwa Rais Teodoro Obiang Nguema ameshinda kiti hicho kwa
kupata asilimia 98 ya kura zilizopigwa.
Hata hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatazamiwa kutoa matokea rasmi Alkhamisi ijayo.Akizungumza Jumapili wakati alipokuwa akipiga kura yake, Rais Nguema mwenye umri wa miaka 73 na ambaye anaongoza muungano wa vyama kumi vya siasa, alisema kuwa ana uhakika kuwa atapata zaidi ya asilimia 90 ya kura katika uchaguzi huo.
Hii ni katika hali ambayo, muungano mkuu wa upinzani nchini humo ulisusia uchaguzi huo wa Jumapili.
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, Novemba mwaka 2011, 99% ya watu katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta waliunga mkono marekebisho ya katiba katika kura ya maoni, lengo kuu likiwa ni kuweka kikomo cha uongozi, kwa rais kutokuweko madarakani kwa zaidi yavipindi viwili.
Rais Obiang Nguema aliingia madarakani takriban miaka 37 iliyopita kwa mapinduzi ya kijeshi, baada ya kuupindua utawala wa kidikteta wa Francisco Macias Nguema ambaye alikuwa mjomba wake.
Baada ya kuhukumiwa na kunyongwa Francisco Macias, Obiang Nguema aliwaahidi wananchi wa Equatorial Guinea kwamba utawala wa kidemokrasia utastawishwa nchini humo.
Post a Comment