Umoja wa Mataifa umeelezea wasi wasi wake kuhusu kuongezeka
taharuki na uhasama wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Maman Sidikou, Mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa
Kongo DR(MONUSCO) amesema hali ya kisiasa na usalama ni tete nchini humo, kutokana na baadhi ya vyama vya kisiasa kuitisha maandamano katika miji ya Kinshasa na Lubumbashi. Amezitaka pande zote za kisiasa nchini humo kujizuia na vitendo ambavyo vitazidi kupandisha joto la kisiasa nchini humo. Hata hivyo ameitaka serikali kutokandamiza haki ya wananchi ya kujieleza na kujumuika sambamba na kufanya maandamano ya amani.
Wapinzani wa serikali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametoa wito wa kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Novemba mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Licha ya serikali ya Rais Joseph kabila kupiga marufuku maandamano, lakini wampinzani siku chache zilizopita walikusanyika katika uwanja wa mashahidi mjini Kinshasa na kusisitiza juu ya udharura wa kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Novemba mwaka huu. Wapinzani hao wamesema kuna haja ya kufanyika mabadiliko katika mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi, uchaguzi mkuu unatakiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu wa 2016. Hii ni katika hali ambayo Kamisheni ya Taifa ya Uchaguzi kwa mara kadhaa imekuwa ikisisitiza kuwa, ni suala lisilowezekana kufanyika uchaguzi mkuu katika wakati uliopangwa, kabla ya kupitia daftari la wapiga kura
Post a Comment