Awe
ni paka wa nyumbani ama yule paka wa mwituni na wanyama wote katika
jamii ya pakaa kama vile simba,ama chui, paka huvutia hisia nyingi sana
kwa mwanadamu.
Video za paka ni maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii.
Je unampenda paka ?
Lakini mapenzi hayo ya paka yamefikia hatu mpya.
Amini
usiamini afisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha
paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao
makuu yake huko Westminster.
Afisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza
imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika
makao makuu yake huko Westminster.
Paka huyo ambaye zamani alinusuriwa alipokuwa
akizurura mitaani katika mji mkuu wa London -- alipewa jina
Palmerston, jina la waziri mashuhuri wa zamani wa mashauri ya nchi za
kigeni wa Uingereza na waziri mkuu karne ya kumi na tisa.
Kituo
cha kuwanusuru wanyama, kimesema kwamba Palmerston, alikuwa mkakamavu na
paka mwenye nguvu, ambaye haikuwa vigumu kwake kuwa na marafiki -- au
maadui, katika makao hayo yake mapya katika afisi ya wizara ya nchi za
kigeni.
Post a Comment