0


nikki wa pili
 BAADA ya kutamba na wimbo wa ‘Baba Swalehe’ mkali wa Bongo Fleva, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’, anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa ‘Sweet Mangi’.

  Katika wimbo huo aliomshirikisha Chidy Benzi, anayepatiwa matibabu baada ya kutumia dawa za kulevya, Nikki kutoka kundi la Weusi amezungumzia kabila la Wachaga kwamba ni wazuri na wanajua kupenda.

“Wengi wanasema wasichana wa Kichaga hawajui kupenda wanawaza fedha, lakini ukisikiliza wimbo wangu utajua namna wanavyopenda kuliko wanavyofikiriwa na wengi,” alisema Nikki.

Post a Comment

 
Top