Jeshi la Marekani
limesema kuwa limetekeleza shambulizi kwa kutumia ndege isiokuwa na
rubani nchini Somalia, ikilenga gari moja lilokuwa limewabeba wanachama
watatu wa kundi la kigaidi la al-Shabab.
Kulingana na msemaji wa
pentagon, aliyelengwa hasa ni Hassan Ali Dhoore ambaye anatuhumiwa
kuandaa mashambulizi ya hivi karibuni ya mabomu katika uwanja wa ndege
wa Mogadishu na katika hoteli moja ambapo raia wa Marekani waliuwawa.
Shambulio
hilo la majeshi ya Marekani limetekelezwa katika eneo la kaskazini mwa
mji wa Jilib, karibu na mpaka wa Kenya na Somalia, huku Marekani ikisema
ingali inatathmini matokeo ya shambulio hilo.
Wapiganaji wa al-Shabab
Shambulizi hilo la hivi karibuni la Marekani
linajiri wiki chache baada ya shambulizi jingine katika kambi ya mazoezi
ya al-Shabab kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani na nyingine
iliokuwa na rubani.
Post a Comment