Utafiti mpya
umebaini kwamba kuna soko linaloendelea kuimarika katika biashara haramu
ya bunduki nchini Libya kupitia mitandao ya kijamii hususan ule wa
Facebook.
Vifaa hivyo vilikuwa vikiuzwa kupitia mitandao ya siri ya makundi ya Facebook.
Uuzaji wa bunduki ni ukiukaji wa sheria za huduma ya mtandao huo na msemaji wa Facebook amesema kuwa wanawataka watu kuripoti kuhusu machapisho kama hayo.
Ripoti hiyo ilizinduliwa na utafiti wa silaha ndogo ndogo na data iliochunguzwa na shirika la utafiti la Armament katika mauzo 1,346.
Watafiti wanaamini kwamba hicho ni kipande kidogo cha biashara yote inayoendelea katika mitandao ya kijamii.
Utafiti huo utatolewa siku ya Alhamisi,lakini BBC Newsnight inasema inamiliki nakala ya utafiti huo.
Kanali Muamar Gaddafi alikuwa mnunuzi mkubwa wa silaha na alidhibiti soko la silaha.
Katika kipindi cha miaka 40 alichokuwa mamlakani,inakadiriwa alitumia dola bilioni 30 kununua silaha.
Post a Comment