Wabunge nchini
Ufaransa wamepitisha mswada ambao unaharamisha watu kulipa ili kupata
huduma ya ngono na kuweka faini ya hadi dola 4,274 kwa wale
watakaopatikana na hatia.
Wale watakaopatikana na hatia pia
watalazimika kupewa mafunzo ya mazingira yanayowakabili
makahaba.Imechukua zaidi ya miaka miaka miwili kupitisha mswada huo
wenye utata kutokana na tofauti zilizopo kati ya mabunge mawili kuhusu
swala hilo.Baadhi ya makahaba waliipinga sheria hiyo wakati wa mjadala wa mwisho.
Waandamanaji 60 walipiga kambi nje ya bunge mjini Paris, walibeba mabango moja likiwa na maandishi yaliosema:''Sina haja ya kukombolewa, nitajikomboa mwenyewe'',kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Muungano wa makahaba wa Strass umesema kuwa hatua hiyo itaathiri maisha ya kawaida ya makahaba wanaodaiwa kuwa kati ya 30,000 na 40,000.
Lakini wanaounga mkono sheria hiyo wanasema itasaidia kukabiliana na mitandao ya ulanguzi wa binaadamu.
Pia itakuwa rahisi kwa makahaba wa kigeni kupata kibali cha kufanyia kazi kwa mda nchini Ufaransa iwapo watakubali kutafuta kazi zisizo za ukahaba.
Umuhimu wa sheria hiyo ni kushirikiana na makahaba
,kuwapatia vibali vya utambuzi kwa sababu tunajua asilimia 85 ya
makahaba ni waathiriwa wa ulanguzi wa binaadamu ,mbunge wa chama cha
kisosholisti Maud Oliver ambaye alifadhili sheria hiyo aliambia chombo
cha habari cha AP.
Post a Comment