CUF kudai haki kwa amani
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesisitiza kuwa kitaendelea na juhudi za kutafuta ki yake kwa hanjia yoyote, lakini ya amani ambayo itaungwa mkono na wananchi wa Zanzibar na kwa kuanzia wametangaza kutoitambua Serikali itakayoundwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
wanayodai ilitokana na kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ambao ulifutwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Maalim Seif alisema hayupo tayari kukaa meza moja na Dk Shein kwa ajili ya kutafuta suluhu ya Zanzibar.
“Sipo tayari kukutana na Shein Ikulu kwa ajili ya mazungumzo ya kuleta amani na utulivu Zanzibar...... nitakutana na yeye kama nani kwa sababu sisi CUF hatutambui ushindi wa Shein katika uchaguzi wa marudio pamoja na serikali yake,” alisema Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Aidha, Baraza Kuu la CUF limepitisha maazimio ya kuunga mkono uamuzi wa Marekani kuinyima Tanzania msaada kupitia Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) hivi karibuni.
Kwa upande wake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa juhudi zake ikiwemo kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi zake za kuleta maendeleo kwa wananchi wake na miradi ya maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Serikali ya Watu wa China ni miongoni mwa nchi marafiki makubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya nchi mbili kuwa Jamhuri viongozi wake walikuwa marafiki wakubwa wakitembeleana na kubadilisha wataalamu.
Post a Comment