WAKALA wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) unahitaji kiasi cha Sh
milioni 300 ili kukamilisha baadhi ya matengenezo yanayohitajika
kufanyika kwa haraka katika vituo vya mabasi kabla kuanza utoaji huduma
ambao serikali imesema utaanza rasmi mwezi ujao.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali
za Mitaa, Kaimu Meneja wa Miundombinu wa Dart, John Shauri alisema
fedha hizo ni kati ya Sh bilioni 3.2 ambazo zinahitajika kukamilisha
sehemu ya kwanza ya Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (BRT).
“Ili mradi huu uanze kufanya kazi tunahitaji kwa haraka kiasi cha
shilingi milioni 300 kwa ajili ya kukamilisha kazi zilizosalia ikiwa ni
pamoja na ujenzi wa uzio, kuajiri watumishi na kufanya kampeni
mbalimbali za kuelimisha umma juu ya mradi huo,” alisema Shauri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment