0

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amelia na sare ya 1-1 dhidi ya Toto African ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara juzi, Uwanja wa CCM Kirumba, akisema

mwamuzi huo alitakiwa kuahirisha mechi ndani ya dakika 20 za mwanzo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Azam FC, Hall alisema walikuwa na vita tatu ndani ya mchezo huo, ya kupambana na hali ya uwanja, waamuzi na wapinzani wao hao, jambo ambalo liliwafanya washindwe kuishinda vita hiyo na kujikuta wakiambulia sare.
“Ni matokeo mabaya kwa upande wetu, lakini kuna sababu kadhaa zimechangia… kwanza ni sehemu ya kuchezea mpira, ingekuwa ni mimi mpira usingechezeka, kwangu mimi baada ya dakika 20 ningeahirisha mchezo huo hata kabla ya sisi kupata bao baada ya mistari ya chaki kutoonekana,” amekaririwa akisema kocha huyo raia wa Uingereza.

Aliongeza; “Wachezaji wangu walishindwa kwenda mbele na mipira kabisa, Sure Boy (Salum Abubakar) alishindwa, Farid Mussa alishindwa, Messi (Ramadhani Singano) asingeweza kucheza kwenye hali hii kwani ilikuwa ni ya kupambana sana. “Waamuzi walishindwa kutenda haki, mara nyingi tulipokuwa tukishambulia alipiga filimbi ya kuotea (offside) au tumefanya madhambi, Wanga aliangushwa ndani ya eneo la 18 lakini hatukupewa penalti, ilikuwa ni ngumu sana kushinda vita tatu.”

Post a Comment

 
Top