0

                                              Kizza Besigye
Mkuu wa kikosi cha polisi nchini Uganda amesema kuwa atawaondoa maafisa wake nje ya nyumba ya kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye mara moja.

Hatahivyo maafisa wa polisi bado wako nje ya nyumba ya kiongozi huyo saa kadhaa baada ya afisa mkuu wa polisi kutoa agizo la kuondoka.

Msemaji mmoja wa polisi ameiambia BBC kwamba maafisa wa polisi wataondoka kwa kujikokota na wengine tayari wameondoka.

Hatahivyo hilo halijathibitishwa.

Kamanda katika eneo amewaambia waandishi alikuwa amepokea onyo na kwamba alikuwa anasubiri agizo la mwisho kuwaondoa maafisa wake.

Waandishi hawakuruhusiwa kuingia ili kumhoji bwana Besigye.

Besigye amekuwa akihudumia kifungo cha nyumbani tangu tarehe 20 mwezi Februari,siku ambayo rais Museveni alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa taifa hilo.

Siku ya Alhamisi Mahakama ya juu nchini Uganda ilitupilia mbali kesi inayopinga uchaguzi wa rais Museveni.

Post a Comment

 
Top