Mamia ya watu
wamekongamana nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa
mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan
Mwanamuziki
huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi
kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo
kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho.
Maafisa
wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka
mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti. Marehemu Papa Wemba
Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini
Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba.Mwanahabari
wa BBC Tamasin Ford anasema kuwa mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi
na kubeba mishumaa ili kutoa heshima kwa nguli huyo wa muziki.
Mkewe Papa Wemba na wasaidizi wake pia walikuwepo.
Post a Comment