Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anahutubia taifa hilo kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba kuhusu ujenzi katika makao yake ya kibinafsi eneo la Nkandla.

Rais Zuma amesema anakubali uamuzi wa mahakama na anajivunia uhuru wa mahakama nchini humo.

Amesema uamuzi wa mahakama hiyo ni wa kihistoria kuhusu uamuzi wa mkaguzi wa hesabu za umma aliyewasilisha kesi dhidi yake mahakamani.

"Mahakama imeamua kwamba uamuzi wa mkaguzi wa hesabu za umma ni wa mwisho na anayetaka kubadili hilo lazima apitie kwa mahakama," amesema Bw Zuma.