Klabu ya soka ya
Barcelona Jumatano ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
kuchapwa mabao 2-0 na Atletico Madrid huku Mabao yote ya Altletico
Madrid yakifungwa na Antoine
Griez-mann na bao la pili likifungwa kwa
mara nyingine na Antoine kwa njia ya penalti .
Katika mchezo mwingine Bayern Munich imefakiwa kutinga nusu fainali baada ya kuitoa Benfica kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 katika mchezo wa jana .
Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Rodriguez na Anderson Souza Conceicao , na magoli ya Bayern Munich yakifungwa na Arturo Vidal na Thomas Muller .
Hivyo Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya Hispania pamoja na Manchester City katika nusu fainali ambayo droo yake itapangwa siku ya Ijumaa.
Post a Comment