Azerbaijan
imetangaza kusitisha mapigano kufuatia kuzuka kwa majibizano makali
yaliyofuatia mapigano kati ya majeshi ya Azerbaijan na Armenia kwenye
eneo linalozozaniwa katika jimbo la Nagomo Karabak.
Wizara ya ulinzi ya Armenia imepuuzilia mbali taarifa hiyo ikiitaja kama ya uwongo.
Makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na Armenia, yanasema kuwa mashambulio kutoka upande wa Azerbaijan yanaendelea hivyo basi hawako tayari kusitisha mapigano hayo.
Wanajeshi 30 wameuwawa.
Eneo hilo la ardhi linalozozaziwa limekluwa likidhibitiwa na kundi moja linalotaka kujitenga linalougwa mkono na Armenia tangu kumalizika kwa mapigano katika eneo hilo mnamo mwaka 1994.
Saa 48 ya makabiliano makali ndio ya kwanza mabaya kushuhudiwa tangu mwaka wa 1994 vita vya miongo miwili vilipomalizika.
Msemaji wa serikali ya Azerbaijan amesema kuwa jeshi lao limeteka vijiji 5 na eneo lenye milima muhimu.
Armenia imepinga madai hayo.
Post a Comment