Mashabiki wa vinara
wa ligi kuu ya Uingereza Leicester City walioingia uwanjani hivi leo
kuishabikia dhidi ya Southampton walipewa kopo la pombe au Kitumbua
mlangoni.
Mashabiki hao wa 'the Foxes' wanaendelea na maandalizi ya kusherehekea ushindi wa taji lao la kwanza la ligi kuu ya Uingereza hususan wakifahamu fika kuwa ushindi leo dhidi ya Southampton unawaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kufanikisha ndoto hiyo kuu.
Leicester wanakabiliana na Southampton katika uwanja wao wa nyumbani wa King Power.
Bw Srivaddhanaprabha, ambaye ameratibiwa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa Jumatatu amesema kuwa alitoa 'Ofa' hiyo kwa mashabiki wote wa Leicester City kwa sababu ya ukakamavu wao na kwa uvumilivu klabu hiyo ilipokuwa katika ngazi ya chini.
Leicester inaongoza kileleni mwa jedwali la EPL kwa zaidi ya alama 4.
Mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Susan Whelan, ameiambia BBC Michezio kuwa bw Srivaddhanaprabha amewasili nchini Uingereza kutoka Thailand ilikujumuika na mashabiki wakati huu muhimu.
Leicester wanakamia kuandikisha historia huku wakiwa wamesalia na mechi 6 pekee msimu huu wa kipekee ukamilike.
Ratiba ya mechi za Leicester zilizosalia :Sunderland: 10 Aprili - A
West Ham: 17 Aprili -H
Swansea: 24 Aprili - H
Manchester United: 1 Mei - A
Everton: 7 Mei - H
Chelsea: 15 Mei - A
Post a Comment