Aliyekuwa wakati
mmoja mlinzi wa mwana wa Gaddafi ambaye baadaye alifanya kazi katika baa
moja nchini Australia ameumwa na nyoka alipokuwa akifanya haja ndogo
msituni.
Raia huyo mwenye umri wa miaka 52 alikuwa akinywa vinywaji pamoja na marafikize baada ya kazi siku ya Jumatano wakati alipotoka ili kwenda haja ndogo.
Bwana Peter alikuwa amemaliza kufanya haja ndogo wakati nyoka huyo alipomng'ata kifundo cha mguu.
Anasema aliona sumu ikimwagika kutoka kwa mguu wake na kuhofia kwamba angefariki.
''Nilimwagiwa sumu kidogo .Iwapo ningemwagiwa nyingi pengine ningekuwa katika jeneza alisema,'' Peters.
Post a Comment