Wanajeshi wa Korea
Kusini wanasema Korea Kaskazini imefyatua kombora la masafa marefu
katika eneo la pwani ya mashariki ndani ya bahari, wakati ambapo rais
Barrack Obama anaongoza kikao cha dunia kuhusu usalama wa Nyuklia mjini
Washington.
Ufyatuaji wa kombora hilo ni wa hivi karibuni katika
msururu wa ufyatuaji unaoendeshwa na Pyongyang ambao umesababisha hali
ya taharuki, baada ya taifa hilo kutekeleza jaribio la zana za kinyuklia
mwezi Januari.
Mkutano wa nuklia
Rais wa Marekani Barrack Obama anasema China na Marekani zitashirikiana kumaliza miradi ya nyuklia ya Korea Kaskazini.
Bwana Xi amezitaka pande mbali mbali kuidhinisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Post a Comment