0

                             Wanawake wajifungue hospitalini sio makanisani
Nchini Nigeria kuna kampeni mpya ya kuhamasisha akina mama wasiwe wakijifungua watoto makanisani

Ni kitendo cha kawaida katika jimbo la Cross River, wanawake wanaamini kwamba mungu atawalinda wakati wa kujifungua kuliko daktari hospitalini.

Wakunga hawa ambao wanapatikana kanisani hawana elimu ya kutosha na vifaa vya uzazi.
Maelfu ya wanawake hufariki wakati wa kijufungua kila mwaka.

Kwa sasa kuna mswada bungeni wa kupiga marufuku kujifungua kanisani.
     Kwa sasa kuna mswada bungeni wa kupiga marufuku kujifungua kanisani.
Mwandishi wa BBC Chris Ewokor aliyemtembelea Daktari Linda Ayade anaongoza kampeni hii, katika jimbo la River anasema ni itikadi iliyokita mizizi hususan vijijini

Katika ukumbi wa kituo cha afya cha Uwanse mjini Calabar, zaidi wa wanawake 300 wamemiminika hapa kumsikiza Dkt Linda Ayade, mwanaharakati wa maswala ya afya, na miongoni mwa mkusanyiko huu ni wanawake wajawazito

DR Ayade anasema msukumo wake ni kuokoa maisha ya mama na watoto wanaozaliwa.
"nimefanya kazi katika hospitali hapa Nigeria kama mhudumu wa afya, nimeshuhudia wanawake wanaokimbizwa hospitalini wakiwa hali mahututi kiasi kwamba hawawezi kusaidika.
IWanawake wanaamini kwamba mungu atawalinda wakati wa kujifungua kuliko daktari hospitalini.
''Mara nyingine wakati wanapofika hospitalini wameshakufa, ni jambo la kawaida, kwa hivyo mimi kama mwanamke na mzazi, nikijua kile hufanyika wakati mama anapofariki, kuacha familia, nimejichukula kuwa jukumu langu la kuchangia vyovyote vile kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua"

Huku Dkt Ayade akitoa wito kwa akina mama watumie vituo vya afya, katika jamii nyingine hapa River State, ibaada inaendelea katika kanisa la Land of Promise, miongoni mwa waumini wengi wao ni wanawake wajawazito, na pembeni mwa kanisa, ni chumba kilichokaa, ndani yake kuna taa ndogo ya mafuta, na hapo ndipo wanawake hupelekwa kujifungua, mkunga pia ndiye mchungaji katika kanisa hili

Mchungaji Indoreyin Sambhor, pia ni mkunga katika kanisa hili la Land of Promise, akiongoza misa, na anasema, tangu akiwa mtoto, aliandamana na mamake na kumsaidia katika harakati za kujifungua kwa wanawake na pia aliomba Mungu sana, na tangu aanze hajawahi shuhudia nguvu kama za Mungu, na kila mwanamke amejifungua salama na Mungu anawasaidia sana
.
Mkuu wa Uajenti wa Afya katika jimbo la Cross River Dkt Betta Edu anasema kuwa serikali inapitisha sheria ya kupiga marufuku wanawake kujifungua kanisani.

Kwa sasa mtandao wa kijamii umebuniwa kuhakikisha kwamba wanawake wajawazito wanatumia vituo vya afya inavyotakikana.

"tunahitaji usaidizi wenye msukumo halali ili tuweze kutekeleza wito kwamba haikubaliki mwanamke yeyote kufariki kutokana na matatizo ya kujifungua ilhali ingezuiliwa"

Mikakati inafanywa kufutiilia mbali janga la maafa wakati wa kujifungua. Dkt Ayade anasema kwamba kwa sasa kuna misaada ya vifaa vya uzazi, na pia wanapeana nauli ya kusafiri hadi hospitalini kwa wanawake wajawazito, nia kuu ni kuwahimiza

Post a Comment

 
Top