Shirika uchunguzi wa jinai la Marekani FBI limejitolea kusaidia maafisa wa polisi nchini humo kufungua simu nyingine ya iPhone.
Polisi katika jimbo la Arkansas walikuwa wanataka kufungua simu iPhone na iPod za vijana wawili ambao wanatuhumiwa kuwaua wachumba wawili, shirika la habari la AP limesema.
Hunter Drexler, 18, na Justin Staton, 15, wanatuhumiwa kuwaua Robert na Patricia Cogdell nyumbani kwao Conway, Arkansas Julai mwaka jana.
Syed Farook na mkewe waliuawa kwa kupigwa risasi baada yao kuwaua watu 14 katika mji huo ulioko jimbo la California, Marekani.
FBI walifanikiwa kufungua simu ya Farook wakisaidiwa na taasisi nyingine, baada ya mvutano baina yao na kampuni inayotengeneza simu hizo, kampuni ya Apple.
Kampuni hiyo ilikuwa imekataa kuwasaidia FBI kufungua simu hiyo ikisema hatua hiyo ingehatarisha au kudhoofisha usalama wa simu za iPhone.
Post a Comment