Mabadiliko ya yaliomo katika mtandao wa instagram yamezua hisia kali miongoni mwa watumizi wake.
Machapisho mengi ya watu maarufu ambao wana wasiwasi kwamba picha zao huenda zisionekane na watu wengi yamewataka wafuasi wao kufungua kitufe cha ujumbe.
Lakini Instagram imesema kuwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.
''Tunasikiliza na tunawahakikishia kwamba hakuna mabadiliko yatakayofanyiwa machapisho yenu kwa sasa'',mtandao huo wa usambazaji picha ulisema katika ujumbe wake wa Twitter.
Hatua hiyo itauweka sawa mtandao huo na ule wa facebook ambao unamilikiwa na kampuni hiyo.
Kwa kufungua kitufe cha ujumbe,wafuasi wa watu hao maarufu watakuwa wakipata ujumbe kila wanapoweka machapisho yao.
Watu maarufu kama vile Kylie Jenner na mwanamitindo Cindy Crawford katika siku za hivi karibuni wamewataka mashabiki wao kufungua vitufe vyao vya ujumbe
Post a Comment