Meneja wa zamani wa Man United, Sir Alex Ferguson anaamini Leicester City wanastahili kutawazwa mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu
Msimu uliopita wote ulikuwa wa wasiwasi kwa Leicester kwani walikuwa wakipigania kutoshuka daraja lakini hali imekuwa tofauti kwa mwaka huu.
Hata hivyo, kutokana na hali na moyo wa kujituma walio onyesha chini ya Claudio Ranieri msimu huu, Ferguson anadhani hakuna timu inayostahili kushinda taji la ligi zaidi ya Leicester.
Ferguson ambaye alinyakuwa mataji 13 ya ligi akiwa na United amesema kwa uwezo mkubwa walioonyesha Leicester hana shaka kuwa wanastahili kushinda taji hilo.
Post a Comment