Mamia ya waokoaji
wakiongozwa na majeshi, wahandisi, matabibu wamekuwa wakifanya kazi
usiku kucha katika mji wa India wa Calcutta kuokoa watu wanaosadikiwa
kunaswa kwenye barabara ya juu iliyoanguka ikijengwa.
Inasadikiwa watu wengi wamefukiwa ambapo hadi sasa tayari watu 23 wamethibitishwaa kufariki na mamia wengine kujeruhiwa ambao wanapatiwa matibabu.
"Kulikuwa na watu wengi waliokuwa wamesimama chini ya bara bara hiyo inayopita juu kwa juu kulikuwa na bajaji na taxi nyingi zote zimefukiwa," anasema mmoja wa walioshuhudia mkasa huo
Mkurugenzi Mkuu wa Kikosi cha Kukabiliana na majanga nchini India O P Singh anasema waokoaji wamekuwa wakikata zege ili kuwafikia watu waliokuwa wamezikwa baada ya kuangukiwa na kifusi.
Kampuni iliyokuwa inajenga barabara hiyo ya juu kwa juu amesema watatoa ushirikiano kwa
maafisa wa upelelezi katika uchunguzi wa tukio hilo. Msemaji wa kampuni hiyo K P Rao anasema bado hawajafahamu nini kilichosababisha
Post a Comment