0



Rais wa Marekani, Donald Trump amekejeli jaribio la kombora la kinyuklia la Korea Kaskazini lililofanyika jana, akidai kuwa ingawa limeshindwa ni dharau kwa China.

Jana, Korea Kaskazini ilidai kufanya jaribio lake la kombora la Nyuklia ambalo Marekani ilidai kuwa lilishindwa hata kuvuka mipaka ya nchi hiyo ndani ya dakika chache tangu lilipofyatuliwa.

“Korea Kaskazini imedharau matarajio ya China na ni dharau ya hali ya juu kwa Rais [wa China], ingawa limeshindwa, jaribio la makombora la leo. Mbaya!,” Tafsiri isiyo rasmi ya Tweet ya Rais Trump.

Trump alisema kuwa angependa sana kuumaliza mgogoro wa makombora ya kinyuklia wa Korea Kaskazini kwa njia ya kidiplomasia, lakini ni vigumu sana kutumia njia hiyo.

Katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika jana jijini New York, wajumbe walilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo zaidi vya kiuchumi na kidiplomasia.

Post a Comment

 
Top