0


Mwanariadha Mkenya, Charles Maroa(36) amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla baada ya kumaliza mbio katika Mashindano ya riadha ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika Jumapili tarehe 26 Februari.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema mwanariadha huyo alipewa msaada wa kufikishwa Hospitali ya KCMC.

Mkenya huyo aliyekuwa akishiriki mbio za Kilomita 21 aliwahishwa Hospitali ya KCMC lakini alipofikishwa madaktari walibaini kuwa alishafariki.
Tupe Maoni Yako Hapa Chini ( Matusi Hapana )

Post a Comment

 
Top