Mkuu
wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida,
Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile
kinachodhaniwa ni upweke.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida
kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa
vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka
nyumbani kwake.
Aidha
kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba
hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza
kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia
gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke
yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba
kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe.
“Huyu
bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu maana mke wake amekuwa akiishi
mbali naye kwa kipindi kirefu sana, amekuwa mpweke kwa muda mrefu mno
huenda hicho ndicho kilichosababisha ajitoe roho yake,” amesema Mjumbe
huyo wa Bodi.
Marehemu
Makala ni mzaliwa wa kijiji cha Ndago, wilayani Iramba na anatarajiwa
kuzikwa leo nyumbani kwake, ameacha mjane na watoto watano.
Post a Comment