0
Saudi Arabia imeionya rasmi Marekani isipitishe muswada wa sheria ambayo itapelekea Saudia kushtakiwa katika mahakama za nchi hiyo kutokana na kuhusika kwake na hujuma za kigaidi za Septemba 11 ,2001 katika miji ya New York na Washington.

Muswada huo wa sharia ambao uko katika Bunge la Congress ukipitishwa utaondoa kinga kwa watawala wa Saudia kufikishwa kizimbani kutokana na kuhusishwa kwao na kitendo cha kigaidi kilichopelekea Wamarekani kuuawa ndani ya ardhi ya Marekani.

Saudia imeonya kuwa muswada huo ukipitishwa basi itauza mali zake zote zilizo Marekani jambo ambalo yamkini likaibua mtikisiko wa kiuchumi Marekani. Imearifiwa kuwa tishio hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Adel al-Jubeir mjini Geneva alipokutana na mwenzake wa Marekani John Kerry.

Jubeir amedai kuwa iwapo muswada huo utapitishwa, wawekezaji watapoteza imani na Marekani. Hii ni katika hali ambayo muswada huo unalenga kuweka wazi nafasi ya Saudia katika hujuma za 9/11.



Aghalabu ya waliotekeleza hujuma hizo walikuwa raia wa Saudia ambao walikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na familia ya ukoo wa Aal Saud unaotawala Saudia.

Rais Obama wa Marekani ambaye hivi karibuni alitembelea Saudia amesema atatumia turufu yake kupinga muswada huo. Familia za walipoteza maisha katika mashambulio hayo zilimwandikia barua Obama na kusema hakuna kisingizio chochote cha kukataa kufichua ukweli.

Post a Comment

 
Top