Kenya imetangaza kuanzisha tathmini kuhusu ni teknolojia ipi ya nyuklia itumike ili kujenga kinu cha nyuklia nchini humo.
Bi.Winnie Ndubai ameliambia Shirika la Habari la Xhinhua kuwa, hadi sasa bado Kenya haijachagua teknolojia gani itatumika kwenye kinu kinachotarajiwa kujengwa, lakini kwamba ukubwa, usalama na maji ndiyo mambo yatakayozingatiwa wakati wa kujenga kinu hicho, na kusema teknolojia inayotafutwa ni ile inayoendana na mazingira ya Kenya.
Kenya inapanga kujenga kinu cha nyuklia kabla ya mwaka 2027, na tayari imesaini makubaliano na nchi kadhaa zenye teknolojia ya nyuklia ili iweze kuchagua teknolojia sahihi inayoweza kutumika.
Mwaka jana Kenya ililiomba Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA kufanya mapitio ya mpango wa Kenya kuhusu matumizi ya nyuklia.
KNEB inasema Kenya inahitaji kumiliki nishati ya nyuklia kwa sababu itamaliza vyanzo vya nishati ambayo huzalishwa kwa maji na mvuke katika kipindi cha miaka 20 ijayo.
Ndubai amesema nishati ya nyuklia ni yenye kutegemewa na itaiwezesha Kenya kuwa na uchumi wa masaa 24.
Post a Comment