0



Ndege ya kivita ya Marekani aina ya B-52 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka kwenye kambi ya taifa hilo eneo la Guam.

Jeshi la Marekani limesema wanajeshi wote saba waliokuwa kwenye ndege hiyo walifanikiwa kuruka salama kutoka kabla ya ndege hiyo kuteketea.

Ndege hiyo ilikuwa imepaa kutoka kituo cha jeshi cha Andersen.

Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha moshi mkubwa ukitanda angani kutoka kwa vifusi vya ndege hiyo.

Ndege hiyo, ambayo hutumiwa kuangusha mabomu, ilitumwa Guam kutoka jimbo la North Dakota na ni sehemu ya juhudi za Marekani za kuendeleza uwepo wake kijeshi katika bahari ya Pasifiki.

Gavana wa jimbo la Guam amenukuliwa na tovuti ya habari ya Kuam akisema kwamba halikuwa shambulio.

Ndege aina ya 5-52 zimetumiwa na Marekani kwa miaka 60 sasa, na zilichangia sana vita Vietnam na Afghanistan.

Guam ni jimbo linalomilikiwa na Marekani eneo la Micronesia, Pasifiki magharibi na hupatikana kilomita 6,000 magharibi mwa Hawaii.

Mwaka 2008, wanajeshi sita walifariki baada ya ndege aina ya B-52 kuanguka karibu na Guam.

Post a Comment

 
Top