Mahakama mjini
Kampala leo inatarajiwa kutoa hukumu katika kesi ambapo wanaume 13
wameshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na
al-Shabaab mwaka 2010.
Kesi hiyo imechukua miaka sita.
Baadhi ya washtakiwa walikuwa wameambia mahakama kwamba waliteswa na maafisa wa ujasusi wa kanda, Marekani na Uingereza.
Lakini mahakama ya kikatiba nchini Uganda ilifutilia mbali madai hayo.
Washtakiwa 13
Washukiwa ni 13 kutoka Uganda, Kenya na Tanzania. Saba ni Waganda, 5 Waenya na mmoja anatoka Tanzania.Wao ni: Bw Habib Suleiman Njoroge, Isa Ahmed Luyima Abubaker Betamatory na Dkt Ismail Kalule.
Wengine ni Suleiman Hijar Nyamandondo, Hassan Haruna Luyima, Hussein Hassan Agade, Bw Idris Magondu, Mohamed hamid Suleiman na Yahya Suleiman Mbuthia.
Kutokea kwa shambulio
Idadi ya wahanga
Watu 74 walifariki katika shambulio hilo na wengine 70 kujeruhiwa. Takriban watu 60 waliouawa ni wa kutoka Uganda. Wenginewaliofariki dunia ni kutoka mataifa ya Ethiopia, Eritrea, India na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na mmoja kutoka Ireland na Marekani.
Kuendeshwa kwa kesi
Kesi ilianza miaka mitano baadaye baada ya kucheleweshwa na hatua ya washukiwa kupinga kupelekwa kwao nchini Uganda na kudai kuteswa na vikosi vya usalama.Lakini Oktoba 2014 mahakama ya kikatiba ilitupilia mbali kesi yao na hivyo kesi kuanza.
Wanashtakiwa makosa ya: ugaidi, mauaji na kuwa wanachama wa kundi la kigaidi.
Jaji wa mahakama kuu aliyesikiliza kesi hiyo ni jaji Alfonso Owiny Dollo.
Post a Comment