ALIYEKUWA mpenzi wa Kristina Brown, Nick Gordon, amedai kwamba uharibikaji wa mimba ulimtesa sana mpenzi wake wakati wa uhusiano wao.
Gordon amedai kwamba katika uhusiano wao walipoteza watoto wawili kwa wakati tofauti kutokana na mimba kuharibika na kusababisha afya ya mpenzi wake ianze kubadilika.
“Mbali na kifo kilichomkuta Kristina, kuna mambo mengi aliyapitia na yalikuwa yakimtesa sana, tuliwahi kuharibikiwa na mimba mara mbili kitu ambacho kilimfanya afya yake ibadilike na kuwa na mawazo mengi.
“Tulikuwa tayari kwa kuoana na tulikwenda hadi sehemu husika kwa ajili ya kupanga tarehe ya kuoana lakini haikuwa hivyo na nitaendelea kumkumbuka daima,” alieleza Gordon.
Post a Comment