Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba leo amesaini mkataba na Sony Music , kampuni kubwa ya muziki inayofanya kazi na mastaa wa dunia kama Beyonce, John Legend na Chris Brown.
Moja ya kazi za mkataba huo ni kumtengeneza Alikiba kweye kiwango cha juu zaidi kimuziki, kibiashara na kugharamia video zake na anaporekodi audio zake, kila anapotoa muziki mpya unaachiwa kwa nguvu ya usimamizi wa Sony Music kwenye masoko makubwa ya muziki kama Marekani, Ulaya na Africa.
Mkataba huo
aliosaini Ali kiba unafanana na ule aliosaini mwimbaji staa wa Nigeria
Davido ambapo unavipengele vya kusababisha kolabo kwa urahisi zaidi na
mastaa wakubwa wakiwemo wa Marekani.
Post a Comment